Na VEANCE JOHN
Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden amesaini mkataba wa kazi zake na kampuni ya vipaji ya huko Los Angeles, kuashiria hatua muhimu katika kuunda maisha yake ya baada ya urais. Utiaji saini huo unaashiria kuungana tena na taasisi inayojihusisha na wasanii na sanaa ya Creative Artists Agency (CAA), ambao hapo awali alifanya nayo kazi kutoka 2017 hadi 2020.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_b396b838f40941d1bbe0a7b55f42fe6c~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_b396b838f40941d1bbe0a7b55f42fe6c~mv2.jpeg)
Wakati wa mkataba wake wa awali na shirika hilo la vipaji, alichapisha kitabu cha kumbukumbu yake, kilichoitwa “Niahidi, Baba”: Mwaka wa Matumaini, Ugumu, na Kusudi”, kilichotoka mwaka 2017.
"Rais Biden ni mmoja wa watu wa Marekani wanaoheshimika na mwenye ushawishi mkubwa katika masuala ya kitaifa na kimataifa," Richard Lovett, mwenyekiti mwenza wa CAA, alisema katika taarifa. Shirika hilo la vipaji pia lina uhusiano na Rais wa zamani Barack Obama na Mke wa Rais wa zamani Michelle Obama.
Bwana Joe Biden mwenye umiri wa miaka 82, amekaa kimya sana kuhusu mipango yake baada ya kazi yake ya miongo mitano katika utumishi wa umma, lakini alipoondoka Ikulu ya Marekani mwezi Januari, aliwahakikishia wafuasi wake akisema; "Tunaondoka madarakani, hatuondoki kwenye vita.”
Ingawa CAA kwa kawaida hufungamanishwa na nyota wakubwa wa filamu na watu mashuhuri sana ( A list artists), sio kawaida kwa shirika hilo kufanya kazi na wanasiasa na vikundi vya utetezi wa masuala ya kijamii.
Comments