Na Ester Madeghe
Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte amekiri kwamba aliunda "kikosi cha kifo" ili kukabiliana na uhalifu alipokuwa meya wa miji mikubwa nchini humo.

Katika ushahidi wake wa kwanza kabla ya uchunguzi rasmi juu ya kile kinachoitwa vita yake dhidi ya dawa za kulevya, rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 79 amesema kikosi hicho kinaundwa na "majambazi", anaowapa amri ya "muueni mtu huyu, kwa sababu wasipofanya hivyo, "nitakuua mimi sasa".
Duterte alishinda urais kwa kishindo mwaka 2016 kwa ahadi ya kuiga kampeni yake ya kupinga uhalifu katika jiji la Davao kwa kiwango cha kitaifa. Vita vya dawa za kulevya nchini Ufilipino vilishuhudia maelfu ya washukiwa wakiuawa katika oparesheni tata za polisi na sasa inachunguzwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.
Nilifanya nilichopaswa kufanya, na ikiwa unaamini au huamini ... nilifanya kwa ajili ya nchi yangu," alisema Duterte katika taarifa yake ya ufunguzi. "Nachukia dawa za kulevya, usifanye makosa ya namna hiyo." Hata hivyo, alikanusha kuwa aliwapa wakuu wake wa polisi ruhusa ya kuwaua washukiwa, akiongeza kuwa "kikosi chake cha kifo" kiliundwa na "majambazi saba... sio polisi".
Comments