Na VENANCE JOHN
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani imepiga marufuku matumizi ya rangi nyekundu nambari 3 katika vyakula, vinywaji na dawa za kumeza. Marufuku hii inakuja, zaidi ya miaka 30 baada ya wanasayansi kugundua kuwa kuna uhusiano wa saratani kwa wanyama unaotokana na rangi hiyo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_3e3c830f97424534880fbaa24bc36b25~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_3e3c830f97424534880fbaa24bc36b25~mv2.jpeg)
Rangi ya kusanidiwa (synthetic) iliyotengenezwa kwa mafuta ya petrol (petroleum) na kemikali inayojulikana kama erythrosine, rangi nyekundu nambari 3 hutumiwa kuwekwa kwenye vyakula na vinywaji vyenye rangi nyekundu inayong’ara ya cherry.
Hatua hiyo inatekelezwa kwa ombi la Novemba mwaka 2022 lililowasilishwa na mashirika mengi ya utetezi na watu binafsi, ikiwa ni pamoja na Kituo cha Sayansi kwa Maslahi ya Umma na Kikundi Kazi cha Mazingira, ambapo rangi hiyo ilihusianishwa na saratani.
Watengenezaji wanaotumia rangi nyekundu nambari 3 katika chakula na dawa zinazomezwa kuanzia jana Januari 15, 2027 mpaka Januari 18, 2028, wanatakiwa kurekebisha bidhaa zao. Rangi nyekundu nambari 3 imeruhusiwa kutumika katika chakula licha ya Kifungu cha Sheria ya Marekani ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya FDA.
Kifungu hicho, kwa sehemu, kinakataza mamlaka ya chakula na usimamizi wa dawa (FDA) kuidhinisha kiongeza rangi ambacho humezwa ikiwa husababisha saratani kwa wanyama au wanadamu wakati wa kumeza." Kwa muda na jadi ya muda mrefu, rangi mbalimbali zimekuwa zikitumiwa kuwekwa kwenye vyakula, dawa na hata vinjwaji ili kuboresha mwonekano.
Comments