top of page

RAYVANNY AACHIA NGOMA MPYA APONGEZA AKISEMA "HONGERA UNAITWA MAMA"

Hongera unaitwa Mama Leo ni baadhi ya mistari (Lyrics) za kwenye wimbo mpya wa msanii wa Bongo Fleva #Rayvanny uitwao "Hongera" ambapo unadaiwa kuwa amemuimbia aliyewahi kuwa mpenzi wake Paula ambaye kwa sasa ni mjamzito.

Hayo yanakuja ikiwa ni siku chache toka Paula na mpenzi wake Marioo waachie picha za Ujauzito kwenye mitandao ya kijamii ambapo wimbo huu ni wazi kuwa ni pongezi kwa EX wake huyo.



Hii si mara ya kwanza msanii kuimba wimbo wa pongezi kwa EX wake kwani hata Juma Jux aliwahi kufanya hivyo kwa aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee baada ya kujifungua mtoto aliyezaa na Rotimi, Jux aliingia studio na kuimba wimbo wa pongezi.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page