![](https://static.wixstatic.com/media/ca9c0e_f74451233b0c41efb275958f1189fca1~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/ca9c0e_f74451233b0c41efb275958f1189fca1~mv2.jpg)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda jumamosi ya leo Aprili 27, 2024 amekutana na kundi la vijana linalo fahamika kwa jina la "Wadudu wa Arusha" nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kufanya mazungumzo mafupi na vijana hao. Ambapo Makonda ameahidi kuandaa tukio maalumu na Wadudu kabla ya sherehe ya Mei Mosi ambayo kitaifa itafanyika Mkoani Arusha.
Makonda pia amewasihi Wadudu kuishi kwa upendo, akiwataka waandae mpango wa kutafuta pesa na kusisitiza kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa yupo tayari kufungua milango kwa Wadudu wa Arusha.
Pia Makonda amewataka Wadudu kuhamasisha wakazi wa Mkoa wa Arusha kushiriki katika sherehe ya Mei Mosi na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Wadudu wamekubali kufanya hivyo mbele ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda.
Comments