top of page
Radio on air

RC SIMIYU APIGA MARUFUKU KUTUMIKISHA WANAFUNZI KWENYE MASHAMBA YA WALIMU...

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi amepiga marufuku utumikishwaji wa wanafunzi katika mashamba binafsi ya walimu mkoani humo.




Kihongosi ametoa kauli hiyo wakati akisikiliza kero za wananchi katika Kijiji cha Mwaukoli Kata ya Kisesa wilayani Meatu.

Amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya wananchi wa Mwaukoli kumueleza kuwa kumekuwepo na changamoto ya utumikishwaji wa wanafunzi katika mashamba binafsi ya walimu katika eneo hilo wakitolea mfano Shule ya Msingi Mwaukoli.

Alipotakiwa kutoa maelezo juu ya tuhuma zilizotolewa na wananchi juu ya utumikishwaji wa wanafunzi katika Shule ya Mwaukoli, Afisa Elimu Kata ya Kisesa, Jibende Kanga alikataa kuwepo kwa tabia hiyo na kwamba hakuwahi kupokea malalamiko yoyote kuhusu tuhuma hizo.

Hata hivyo, Mchungaji Lucas Ruvanga wa Kanisa la Adventista la Wasabato katika Kijiji cha Mwaukoli alitoa ushuhuda wa namna ambavyo watoto katika eneo hilo wamekuwa wakitumikishwa.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page