top of page

RIDHIKI NI KEKI KUBWA KILA MTU ANAMEGA KIPANDE CHAKE..




Kutoka kwenye ukurasa wa Mtangazaji Kinara wa soka Baraka Mpenja kutoka Azam TV amefunguka ujumbe huu

Ukiona unapata hisia za maumivu unapoona Mtu mwingine anafanikiwa, kaa chini, muombe sana Mungu akuondolee roho ya Wivu na tamaa!.

Mtu mwingine kufanikiwa hakuathiri chochote katika maisha yako, riziki hupangwa na Mwenyezi Mungu.

Riziki ni Keki kubwa, kila mtu anamega kipande chake, ridhika na kile ulichonacho, mafanikio ni hatua zako mwenyewe, usijilinganishe na Mtu mwengine.

Vijana wenzangu, tufanye kazi kwa bidii kubwa, tupunguze maneno na kujisifu maana maandiko matakatifu katika Biblia yanasema ajikwezae atashushwa na ajishushae atakwezwa.

Jitume kufanya kazi, kuwa mvumilivu na mafanikio yako yatapiga kelele, Watu wataona, watakutambua na kukupa heshima unayostahili.

Ukiona unatumia saa moja kueleza wewe ni nani?, ujue bado hujafanya kazi, kwa kawaida mafanikio yana tabia ya kupiga kelele, watakujua tu ukifanya kazi kwa ufanisi na maarifa.

Pokea kidogo busara za Mwamba wa Umalila!" Mpenja.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page