top of page

RIPOTI: 2024 NDIO MWAKA MBAYA ZAIDI KATIKA HISTORIA KWA WAANDISHI WA HABARI, ISRAEL IMEUA IDADI KUBWA ZAIDI

Na VENANCE JOHN


Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) imesema mwaka 2024 ulikuwa mwaka mbaya zaidi katika historia iliyorekodiwa kwa waandishi wa habari waliouawa.


Ripoti hiyo imeonesha kwamba nchi ya Israel ndiyo matukio ya kuuawa kwa waandishi habari yametokea sana kwani asilimia 70 ya waandishi 124 waliopoteza maisha mwaka jana yaklitokea nchini humo. Taarifa iliyotolewa jana na CPJ imesema kuwa mwaka 2024 ulikuwa mwaka mbaya zaidi tangu shirika hilo lianze kutunza kumbukumbu huku waandishi wa habari 124 wakiuawa kote duniani.


CPJ imesema ongezeko la mauaji ya waandishi habari duniani asilimia 22 kutoka mwaka 2023 limetokana kwa kiasi kikubwa katika vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza. Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) imesema: "Takriban waandishi wa habari 85 wameuawa wakati wa vita vya miezi 15 vya Israel huko Gaza, na kwamba wote wameuawa na askari wa Israel, 82 kati ya waandishi hao wa habari walikuwa Wapalestina.


Hata hivyo, Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali ya Gaza inasema idadi ya waandishi wa habari waliouawa na Israel ni kubwa zaidi ya takwimu za CPJ. ikisema waandishi habari 205 waliuawa huko Gaza tangu tarehe 7 Oktoba 2023.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page