top of page

ROBERT KENNEDY MGOMBEA URAIS WA KUJITEGEMEA AJIONDOA, AAMUA KUMUUNGA MKONO TRUMP

Na VENANCE JOHN


Mgombea wa urais nchini Marekani ambaye ni wa kujitegemea wa uchaguzi Robert F. Kennedy Jr amesitisha kampeni yake na kutangaza kumuunga mkono Donald Trump wa chama cha Republican.

Robert F. Kennedy Jr ni mtoto wa Robert F. Kennedy Sr aliyewahi kugombea urais kwa tiketi ya Democrat lakini akauawa na ni mpwa wa aliyekuwa Rais wa Marekani kupitia chama cha Democrat John F. Kennedy. Hatua hiyo inahitimisha jaribio lake la kuingia Ikulu ya White House ambalo lilianzia katika chama cha Democrats.


Kennedy amesema alikutana na Trump na washirika wake mara kadhaa na kugundua kuwa walikubaliana kuhusu masuala kama vile usalama wa mpakani, uhuru wa kujieleza na kumaliza vita.


Kennedy amesema ataondoa jina lake kutoka karatasi za kupigia kura katika majimbo 10 yenye mchuano mkali yanayoweza kuamua matokeo ya uchaguzi wa Novemba 5, na atabaki kuwa mgombea katika majimbo mengine.Watalaamu wa mikakati wanasema haijabainika kama uamuzi wa Kennedy utamsaidia Trump, ambaye yuko katika mchuano mkali na makamu wa rais Kamala Harris.


Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page