top of page

RUTH CHEPNGETICH MWANARIADHA WA KENYA AVUNJA REKODI YA DUNIA

Na VENANCE JOHN


Mwanariadha wa Kenya Ruth Chepngetich amevunja rekodi ya dunia kwa kushinda mbio za masafa marefu za Chicago Marathon hapo jana Jumapili.


Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 ametumia muda wa saa mbili, dakika tisa na sekunde 57 na hivyo kupita rekodi ya awali ya Tigst Assefa wa Ethiopia kwa karibu dakika mbili.

Chepngetich ndiye mwanamke wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili na dakika 10. Assefa aliweka rekodi ya awali kwa ushindi wa Berlin Marathon mwaka 2023 kwa saa mbili, dakika 11 na sekunde 53.


"Ninajisikia vizuri sana, ninajivunia. Hii ni ndoto yangu ambayo imetimia," alisema Chepngetich, bingwa wa dunia wa marathon 2019 na kuongeza kuwa amepambana sana akifikiria rekodi ya dunia na sasa ameitimiza. Ushindi kwa Chepngetich ni wa tatu kwake huko Chicago Marekani ambapo alishindwa kuvunja rekodi ya dunia ya wakati huo ya Brigid Kosgei kwa sekunde 14 mwaka 2022 .

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page