top of page

RWANDA KUANZISHA KODI KWA MAKANISA, RAIS KAGAME AONYA WACHUNGAJI WANAOWAFILISI WAUMINI

Na VENANCE JOHN


Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema kuongezeka kwa makanisa mengi ambayo ameyashutumu kwa kile alichosema viongozi wa madhehebu yamekuwa yakichukua fedha za waumini. Kagame amesema fedha za waumini zinawatajirisha viongozi wa madhehebu na kwamba hali hiyo itailazimu serikali kuanzisha kodi ya makusanyo ya kanisa.


Rais Kagame amesema makanisa hayo yanayoibuka yamekuwa yakifanya alichokiita unyang'anyi wa mpaka senti za mwisho za watu masikini na hivyo kunahitajika udhibiti wa hali hiyo. Mpaka sasa, serikali ya Rwanda imeshafunga makanisa zaidi ya 5000 kwa kile kinachotajwa kwamba ni kutozingatiwa kwa kanuni za usalama, na kukiuka sheria.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page