top of page

RWANDA KUSITISHA PIKIPIKI ZINAZOTUMIA PETROLI

Na VENANCE JOHN


Serikali ya Rwanda imesema kuwa kuanzia mwaka 2025 pikipiki ambazo hazitumii nishati ya umeme hazitasajiliwa. Hii ni safari ya Rwanda kuanza kuondoa katika matumizi pikipiki zinazotumia mafuta kwa nia ya kusafisha mazingira na hewa.


“Hatutasajili pikipiki za petroli kwa usafiri wa umma mjini Kigali. Ni zile za umeme pekee ndizo zitakazozingatiwa kwa usafiri wa umma wa kibiashara,” Jimmy Gasore, Waziri wa Miundombinu aliwaambia waandishi wa habari. Waziri alifafanua kuwa sera hiyo haitaathiri pikipiki zilizopo zinazotumia mafuta ya petroli, ambazo zitaendelea kufanya kazi bila usumbufu.


Naye Juliet Kabera, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Rwanda (REMA), alisisitiza faida za kimazingira, akibainisha kuwa pikipiki za umeme zinachangia kutotoa hewa chafu.


Nchi nyengine pia zimeonyesha nia kama ya Rwanda kwani, mwaka 2023 Rais wa Kenya William Ruto alizundua kiwanda ambacho kinatengeza pikipiki za umeme akisema kuwa matumizi ya pikipiki hizo yatahimizwa kwa ajili ya kuchangia hewa safi nchini humo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page