top of page

RWANDA MBIONI KUIDHINISHA UZAZI WA MPANGO KUANZIA UMRI WA MIAKA 15

Na Ester Madeghe,


Waziri wa Afya wa Rwanda amewasilisha muswada unaolenga kuwaruhusu wasichana wenye umri wa miaka 15 na zaidi kupata huduma za afya ya uzazi, hasa uzazi wa mpango, ili kupunguza mimba zisizotarajiwa. "Sheria inayodhibiti huduma za afya", iliyowasilishwa Bungeni Jumanne, itajadiliwa na kupigiwa kura katika siku zijazo, ili kuona sauti zinazoupinga mpango na zinazokubaliana nao.


"Kutofikiwa kwa huduma za afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na uzazi wa mpango, kunasababisha viwango vya juu vya mimba zisizotarajiwa", Waziri wa Afya Sabin Nsanzimana amesema wakati akiwasilisha mradi huo kwa wabunge.


Watetezi wa mpango huo pia wanahoji kuwa sheria ya sasa inawabagua wasichana waliobalehe kwa kuwanyima haki ya kufanya maamuzi kuhusu afya yao ya uzazi, kwani takwimu zinaonyesha umri wa watu wengi wanaofanya ngono au wanaojiingiza katika mahusiano ya kimapenzi nchini Rwanda ni miaka 18.


Mnamo mwaka 2022, Bunge la nchini Rwanda, lilikataa mpango huo, ulioandaliwa na Aflodis Kagaba, mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la "Initiative for the Development of Health", ambalo lilishiriki katika kuandaa muswada huo.


"Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu bado hawako wazi juu ya wazo hilo," Aflodis Kagaba ameliambia shirika la habari la AFP, huku akionyesha kwamba amefanya "utafiti mwingi na ukweli unaoonyesha kwamba vijana wanashiriki ngono na kwamba tunahitaji kulinda".


"Sitaupigia kura mswada huu. Mtu mwenye umri wa miaka 15, bado ni mtoto, lakini kwa sheria kama hiyo, watu wazima watawanyonya kwa urahisi na kuwanyanyasa kingono bila matokeo," mbunge Christine Mukabinani, kutoka chama cha PS Imberakuri ameliambia sjirika la habari la AFP.


Kulingana na Wizara ya Afya, Rwanda inashikilia rekodi ya kuwa kinara dhidi adha ya mimba za utotoni. Kati ya mwezi wa Januari na Juni 2024, zaidi ya mimba 10,000 za mapema zimerekodiwa. Kadhalika, utoaji mimba nchini Rwanda ni halali, ikiwa tu ni matokeo ya ubakaji au ndoa ya kulazimishwa.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page