top of page

RWANDA YAZIPITA TANZANIA NA KENYA KWA UNAFUU WA HUDUMA YA INTANETI

Takwimu kutoka kampuni ya utafiti ya teknolojia ya Uingereza Cable zinaonesha kuwa wastani wa gharama ya mtandao wa Intaneti nchini Rwanda imepungua kutoka dola za Marekani 60.96 sawa na Tsh 152400 mpaka dola 43.22 sawa na Tsh 108050 kwa mwezi.





Kupungua huko kwa asilimia 29.1% sio tu kwamba kunaifanya Rwanda kuwa mfano wa azma yake ya kuimarisha upatikanaji wa intaneti bali pia kunaonesha mwelekeo wa kupungua kwa gharama ya inteneti kwenye nchi zinazoendelea.


Tanzania, ambayo hapo awali ndiyo ilikuwa inaongoza chati ya uwezo wa kumudu, inaonekana kuwa na ongezeko kidogo la wastani wa gharama, ambayo sasa inafikia dola za Marekani 43.44 sawa Tsh 108600 kwa mwezi. Wakati huo huo, bei ya mtandao wa intaneti nchini Kenya imeshuka kidogo kutoka dola 49.13 sawa na Tsh 122825 mpaka dola 47.73 sawa na Tsh 119324.9


Mabadiliko haya yanaonesha mazingira ya ushindani ambapo bei za watumiaji huathiriwa moja kwa moja na mienendo ya soko na ushindani baina ya nchi. Mdau wetu unaweza kutwambia, ulishawahi kupiga hesabu ukajua, kwa mwezi unatumia kiasi gani kununua vifurushi vya intaneti?

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page