Na VENANCE JOHN
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) inatarajia kukutana leo katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, kwa mkutano wa kilele wa kipekee kuhusu hali ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Taarifa hiyo imetolewa na katibu mkuu wa SADC, Elias Magosi hapo jana Alhamisi.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_536371cb09ba44c5a966b440366c0d99~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_536371cb09ba44c5a966b440366c0d99~mv2.jpeg)
"Mkutano huu usio wa kawaida unalenga kujadili masuala yanayohusiana na Mashariki mwa DRC, hali ambayo inatia wasiwasi kufuatia kutekwa kwa siku za hivi karibuni kwa Goma, jiji kuu la mkoa wa Kivu Kaskazini, na kundi la waasi linaloipinga serikali, M23 na vikosi vya Rwanda, Elias Magosi amesema.
Wanajeshi kadhaa wa kigeni kutoka Afrika Kusini na Malawi waliouawa katika mkoa wa Kivu Kaskazini wiki iliyopita ambao walikuwa sehemu ya kikosi cha SAMIDRC kinachopiga kambi karibu na Goma.
Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi amewarai vijana kujiunga kwa wingi na jeshi la taifa kusaidia kupambana na waasi wa M23 wanaojaribu kukamata maeneo makubwa zaidi mashariki mwa nchi hiyo.
Comments