top of page
Radio on air

SAMAKI WENGINE WAINGIA MTONI LORI LIKIPATA AJALI

Lori lililokuwa limebeba samaki walio hai wapatao 102,000 nchini Marekani, limepata ajali kwenye korongo moja na kusababisha idadi kubwa ya samaki hao kuingia mtoni.




Samaki hao wadogo, walikuwa wametolewa kutoka mahali walipozalishwa ili kupelekwa katika mto Amaha, kwa sababu idadi yao imepungua sana katika mto huo.

Lakini ajali ilitokea kabla ya kufika huko na kusababisha samaki wapatao 77,000 kuingia katika mto mwingine kwenye korongo la Lookingglass, na badala yake kuongeza idadi kwenye mto huo.

Licha ya idadi kubwa kuweza kuingia ndani ya maji samaki wengine hawakuwa na bahati na waliishia kuangukia kwenye kingo za mto huo (picha ndogo).

Maafisa wa wanyamapori wamesema siku ya Jumanne kuwa dereva alipoteza mwelekeo kwenye kona kali na kusababisha lori hilo kuporokoma korongoni. Dereva huyo alipata majeraha madogo, idara ya samaki na wanyama ya Oregon ilisema kwenye taarifa yake.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page