Na Nassor Nangi.
Baada ya muda mrefu hatimaye kampuni ya Samsung yaifichua rasmi pete yake ya kwanza,
![](https://static.wixstatic.com/media/146e6d_7f2e2d04d3bc4a74bbb3717138c8583b~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/146e6d_7f2e2d04d3bc4a74bbb3717138c8583b~mv2.jpg)
Pete ya Galaxy (GALAXY RING), yenye bei ya $399 ambayo ni takribani shilingi milioni 1,065,308/= za Tanzania, ambayo itazinduliwa mnamo Julai 24, 2024.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ripoti ya jarida la mtandaoni la 'Wealth' Pete hiyo itakayokua ikivaliwa vidoleni, itasaidia ufuatiliaji wa afya, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa ubora wa usingizi, kupima mapigo ya Moyo na uwezo wa kudhibiti simu yako ya kiganjani.
Hii itakua ni moja ya kifaa cha kielektroniki kidogo zaidi kinachoweza kuvaliwa kutoka kwenye kampuni ya Samsung hadi sasa, Galaxy Ring inahimiri wiki moja ya matumizi ya betri kwenye pete hiyo kwa kuichaji mara moja tu, ikitofautisha na vifaa vingine vya aina yake.
Comments