top of page

SANAMU YA RAIS MSITAAFU WA GHANA AKUFO-ADDO YAHARIBIWA, YATENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI

Na VENANCE JOHN


Sanamu ya aliyekuwa Rais aliyemaliza muda wake hivi karibu wa Ghana, Nana Akufo-Addo, imeharibiwa. Sanamu hiyo iliwekwa mwishoni mwa mwaka jana. Ilizinduliwa na na yeye mwenyewe Akufo-Addo mwezi Novemba, 2024 katika Mkoa wa Magharibi wa nchi hiyo na kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na kukejeliwa na kuelezewa kama kujitukuza.


Siku ya jana Jumatatu, vyombo vya habari vya ndani vilichapisha picha inazoonesha sanamu hiyo ikiwa katika hali iliyoharibiwa, na kichwa chake kilichokatwa kikiwa chini. Mpaka sasa haijabainika ni nani aliyelenga sanamu hiyo au alikuwa na nia gani. Kiwiliwili pia kinaonekana kuharibiwa, na msingi ulioharibiwa tu ndio unabaki mahali hapo ilipokuwa zamani.


Akufo-Addo alijiuzulu kama rais wiki iliyopita ili kumoisha rais mpya, baada ya kuhudumu kwa mihula miwili madarakani baada ya mgombea wa chama chake kushindwa vibaya katika uchaguzi wa urais wa mwezi Desemba. Uharibifu wake umezua hisia tofauti. Mkazi mmoja amekiambia kituo cha redio cha Citi FM kwamba, sanamu hiyo haikuwa na faida kwa watu, kwa hiyo ikiwa imeharibiwa, ni kawaida.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page