top of page

SASA NI RUKSA KUISHI KENYA MIEZI 6 BILA KIBALI CHOCHOTE KWA WAAFRIKA, ISIPOKUWA LIBYA NA SOMALIA

Na VENANCE JOHN


Kulingana na agizo jipya la baraza la mawaziri, Kenya itawaruhusu raia wa takriban mataifa yote ya Afrika kuzuru nchi hiyo bila kuhitaji idhini ya awali.


Chini ya mfumo uliorekebishwa, raia wa nchi nyingi za Afrika wataruhusiwa kuingia Kenya na kukaa bila kuhitaji Idhini ya Usafiri wa Kielektroniki (ETA) kwa hadi miezi miwili. Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo ni pamoja na Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi, wanaweza kukaa hadi miezi sita kulingana na sera ya umoja huo.


Mwaka jana, Kenya ilianzisha sera ya "bila visa" ambayo ilihitaji wageni wengi kutuma maombi mtandaoni ili kupata idhini kabla ya kuingia nchini humo. Lakini kuanzishwa kwa Idhini ya Usafiri wa Kielektroniki (ETA), ambayo ilichukua nafasi ya hitaji la visa kwa wageni wote, lilikosolewa kwani lilionekana kama visa mpya lakini kwa jina lingine.


Siku ya Jumanne, taarifa ya baraza la mawaziri ilisema Idhini ya Usafiri wa Kielektroniki (ETA) itaondolewa kwa nchi zote za Afrika isipokuwa Somalia na Libya kutokana na wasiwasi wa usalama. Taarifa hiyo ilisema hiyo ni sehemu ya juhudi za kuunga mkono sera za ukuaji wa utalii na kukuza ushirikiano wa kikanda na kurahisisha usafiri katika bara zima.


Nchi kadhaa za Afrika zimejaribu kurahisisha mahitaji ya usafiri kwa wageni kutoka kwingineko barani humo katika miaka ya hivi karibuni, huku tafiti zikionyesha mara nyingi ni rahisi kwa raia wa nchi za Magharibi kutembelea nchi za Afrika kuliko Waafrika kutembeleana.


Mapema mwaka huu, Ghana nayo ilisema wamiliki wote wa pasipoti za Kiafrika sasa wataweza kuzuru bila kuhitaji visa. Wageni wa Kiafrika wanaotembelea Rwanda pia hawahitaji visa kuingia nchini humo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page