Na VENANCE JOHN
‘Seabright’ ndiyo jina walilopewa kuku hawa wenye asili ya Uturuki. Kuku hawa wanatumika zaidi kwa ajili ya urembo na mapambo lakini baadhi ya watu wanawatumia kwa ajili ya biashara na wengine kwa ajili ya kitoweo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_9b0e2998106c4bbc9692c43e7d217482~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_9b0e2998106c4bbc9692c43e7d217482~mv2.jpg)
Tovuti ya Livestock conservancy ya masuala ya mifugo, kuku hao wana urefu wa sentimita 33 (rula moja) na uzito wa kuanzia gramu 500 (nusu kilo /0.5kg ) kwa tetea (kuku anayetaga) na majogoo hufikia hadi gramu 600 (0.6kg).
Kuku hao wana uwezo wa kutaga wakiwa na miezi 7, kadhalika jogoo nao wanaweza kuwika wakiwa na miezi saba.
Seabright wanaweza kutaga mayai 60 mpaka 80 kwa mwaka yanayoweza kuongezeka au kupungua kutoka kwa kuku mmoja hadi mwingine huku wakiwa na uwezo mdogo wa kulalia hadi kuyatotoa.
Credits :Nukta
See less
Comments