top of page

SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA 2,611, NYINGI ZIKIWA ZA UALIMU

Na VENANCE JOHN


Serikali imetangaza nafasi 2,611 za ajira ambapo kati ya nafasi hizo asilimia 98 ni za walimu wa kada mbalimbali. Katika tangazo hilo lililotolewa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma limesema mwisho wa kutuma maombi hayo ni Februari 20, 2025.


“Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi elfu mbili mia sita kumi na moja (2,611) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili,”imeeleza sehemu ya tangazo hilo.


Nafasi hizo ambazo kiwango kikubwa ni za ualimu, pia kada nyingine zipo kwa uchache ikiwamo zile za huduma kwa jamii na uhandisi. Sekreterieti ya ajira imesema waombaji wote wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia mfumo wa kieletroniki wa ajira kwa njia ya mtandao wa intaneti (Recruitment Portal).

Kommentare


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page