top of page

SGR YA MIZIGO KUANZA MWEZI UJAO

Na VENACE JOHN


Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema linatarajia kuanza kusafirisha mizigo kati ya kuanzia Januari hadi Machi mwakani na kwamba mabehewa 264 ya mizigo ya reli ya kisasa (SGR) tayari yapo Bandari ya Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amesema kazi ya kuyashusha mabehewa hayo tayari imeanza na mwezi ujao wataanza kusafirisha mizigo kutoa Dar es salaam mpaka Dodoma. Kadogosa amesema katika kipindi cha Baragumu Live kinachorushwa na kituo cha runinga ya Channel Ten.


Amesema treni ya mizigo itakapoanza wafanyabiashara wanaweza kuingia mkataba na shirika hilo kuhakikisha mizigo yao inafika kwa muda na siku iliyopangwa. “Mikataba itasaidia kuwa na uhakika wa kusafirisha mizigo ndani ya siku au saa kadhaa. Tunafahamu kwamba wafanyabiashara wanaisubiri kwa hamu treni hii,’’ amesema Kadogosa.


Hata hivyo Kadogosa amesema treni hiyo ya mizigo haibeba mizigo inayobebwa na malori, badala yake watajenga bandari kavu ambayo itakuwa kituo cha kushusha mizigo hiyo na malori kuipeleka katika maeneo husika.

Kommentare


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page