top of page

SHERIA YA ILIYOPENDEKEZWA YA KUSAIDIWA KUFA UINGEREZA KUBADILISHWA ILI KUONDOA UTIAJI SAINI WA MAJAJI

Na VENANCE JOHN


Pendekezo la sheria mpya ya Uingereza ya kusaidiwa kufa kwa wagonjwa mahututi itarekebishwa ili kuondoa sharti kwamba jaji wa Mahakama ya Juu atie sahihi katika kila kesi. Wapinzani wa sheria ya kusaidiwa kufa wanasema mabadiliko hayo yatadhoofisha ulinzi wa kuwalinda watu walio hatarini dhidi ya kulazimishwa au kushinikizwa kujiua.


Katika kura ya kihistoria miezi mitatu iliyopita wabunge waliunga mkono muswada huo wa kuruhusu kusaidiwa kufa, na kufungua njia kwa Uingereza kufuata nchi nyingine kama vile Australia, Canada na baadhi ya majimbo ya Marekani.


Chini ya mapendekezo hayo, watu wazima wenye uwezo wa kiakili, wagonjwa mahututi nchini Uingereza na Wales walio na miezi sita au chini ya hapo kuishi watapewa haki ya kuchagua kukatisha maisha yao kwa usaidizi wa matibabu baada ya kuidhinishwa na madaktari wawili na hakimu.

Σχόλια


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page