top of page

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU DUNIANI (FIFA) LAOMBWA KUSITISHA KOMBE LA DUNIA KUCHEZWA SAUDI ARABIA

Na Ester Madeghe,


Mashirika ya kutetea haki za binaadamu yamelitaka Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA kusitisha mchakato wa kuichagua Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa michuano ya soka ya Kombe la Dunia mwaka 2034, kutokana na kulalamikiwa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu.


Mashirika hayo yametaka mapendekezo ya kombe la dunia kuchezwa Saudi Arabia kusitishwa haraka, mpaka pale Saudi Arabia itakapotangaza mageuzi makubwa ya haki za binaadamu kabla ya maamuzi magumu kufikiwa.


Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema yamefanya tathmini kuhusu mikakati ya haki za binaadamu iliyopendekezwa na mataifa yaliyoomba kuwa mwenyeji wa michuano hiyo na kuhitimisha katika ripoti mpya kwamba hakuna pendekezo lililoainisha namna ya kufikia viwango vya haki za binaadamu vinavyotakiwa na FIFA. Aidha, mashirika hayo yameongeza kuwa, tishio kubwa lipo Saudi Arabia na kwamba michuano hiyo nchini humo ni wazi itakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za bidaadamu.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page