Na VENANCE JOHN
Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT) limeeleza kusikitishwa na hatua ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kumfungia Samuel Eto’o, rais wa shirikisho la kandanda nchini humo kushiriki katika mechi za timu ya taifa hilo kwa kipindi cha miezi sita.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_6b4fca728a054a0ebd802f4e7462fe7f~mv2.jpg/v1/fill/w_526,h_526,al_c,q_80,enc_avif,quality_auto/57c8da_6b4fca728a054a0ebd802f4e7462fe7f~mv2.jpg)
Jumatatu wiki hii, FIFA ilisema imemzuia mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Barcelona baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka kanuni za usawa katika mchezo na kuwatendea vibaya wachezaji na maofisa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia, kwa Wanawake chini ya miaka 20, katika mzunguko wa 16 uliohusisha mechi kati ya Brazil na Cameroon, mwezi Septemba.
Eto’o amekuwa akikumbwa na masakata mengi yanayohusisha kukiuka kanuni za soka, kwani shirikisho la kandanda Afrika CAF liliwahi kumkuta na hatia ya kukiuka maadili kwa kuwa na mkataba na kampuni ya kubashiri kinyume na miongozo kwa viongozi wa soka kujihusisha na makampuni ya kubashiri (Betting companies).
Comments