Na VENANCE JOHN
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamaganda Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwaandikia barua klabu ya Simba SC baada ya kung'olewa kwa viti katika uwanja wa taifa (Uwanja wa Benjamin Mkapa) katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika uliofanyika kati ya Simba SC dhidi ya wangeni wao CS Sfaxien ya kutoka Tunisia.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_70f2591fc5f84af2b8a412369b8dc263~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_70f2591fc5f84af2b8a412369b8dc263~mv2.jpeg)
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini wa Wizara hiyo, imesema barua hiyo itakayoandikwa na kupelekwa kwa Simba SC nakala nyingine itatakiwa kwenda kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu huo zilipwe. Vurugu ziliibuka jana Desemba 15, 2024 katika mechi baina ya Simba dhidi ya CS Sfaxien, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Baada ya vurugu hizo kutokea, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema viti 256 viling'olewa katika vurugu hizo. Pia shabiki mmoja wa timu ya CS Sfaxien anadaiwa kuumia na kupatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa, huku viti vya rangi ya bluu 156 na machungwa 100 viking'olewa na mashabiki.
Comments