top of page

SIMBA SC NA AZAM FC KUSHIRIKI KOMBE LA MUUNGANO UPANDE WA BARA KUANZIA APRILI 23...

Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wametoa taarifa hii

"Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa pamoja, tunatangaza kurejea tena kwa Kombe la Muungano baada ya miaka 20 kupita,



kipekee kabisa Kombe hilo limerejea rasmi katika wakati ambao, Taifa linasherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wetu.

Timu za Simba SC na Azam FC kutoka Tanzania Bara, zitashiriki katika Mashindano hayo ya mwaka huu yenye sura ya Uzinduzi wa Kombe hilo, huku kwa upande wa Visiwani timu shiriki ni mabingwa wa Zanzibar, KMKM pamoja na KVZ FC.

Mechi hizo zitachezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia Aprili 23.

TFF na ZFF tunawaomba Watanzania wote kushirikiana ili kufanikisha mashindano haya kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu."


Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page