Taarifa iliyotolewa na klabu ya Simba SC inaeleza kuwa
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_3f537abde8dd4254ad54e85ae13def84~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_3f537abde8dd4254ad54e85ae13def84~mv2.jpeg)
"Tunapenda kuutarifu umma kuwa Klabu ya Simba, imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Ndugu Francois Regis, ambaye alikuwa ni Mtendaji Mkuu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunamshukuru Mr. Regis kwa kipindi alichohudumu katika Klabu yetu. Bodi imefanya uteuzi wa Bi. Zubeda Hassan Sakuru kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.
Bi. Zubeda yuko mbioni kuhitimu Shahada yake ya kwanza ya Uzamivu, ana Shahada mbili za Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania. Pia ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Bi. Zubeda amefanya kazi kama Meneja Miradi wa Simba akimsaidia Bw. Kajula kuhusu mchakato wa kutengeneza sera na ushauri wa masuala ya kiutendaji. Tafadhali ungana nasi kumtakia heri Regis na kumkaribisha Zubeda katika Klabu ya Simba."
Comentários