top of page

TALIBAN YAPIGA MARUFUKU WASICHANA KUPIGA SIMU VITUO

TALIBAN YAPIGA MARUFUKU WASICHANA KUPIGA SIMU VITUO VYA REDIO NA TELEVISHENI...

Shirika la Waandishi wa Habari la Afghanistan linasema mamlaka ya Taliban katika jimbo la



Khost imepiga marufuku wasichana kupiga simu kwenye vituo vya redio na televisheni.

Taliban pia imevionya vyombo vya habari vya ndani kutokupokea simu kutoka kwa wasichana.

Tarifa hiyo ilidai kwamba mawasiliano kama hayo yanaweza kusababisha "tabia isiyofaa" ambayo inaweza kukiuka tafsiri ya Taliban ya sheria za Kiislamu.

Tangu kuchukua mamlaka mnamo Agosti 2021, Taliban imeweka vikwazo kadhaa kwa wanawake na wasichana.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page