top of page

TIKTOK KUNUNULIWA NA MICROSOFT

Na VENANCE JOHN


Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa kampuni ya Microsoft iko kwenye mazungumzo ya kuununua mtandao wa TikTok.


Trump amesema kwamba angependa kuona ushindani wa zabuni katika mchatako wa uuzaji wa programu hiyo ya mitandao ya kijamii ambayo kampuni yake mama ni Bytedance. Trump alipoulizwa na waandishi habari iwapo kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ya Marekani ilikuwa ikijitayarisha kuinunua tiktok, Trump alijibu; "Naweza kusema ndiyo.


Trump na mtangulizi wake Joe Biden wamekuwa wakijaribu kwa miaka mingi kulazimisha kampuni mama ya TikTok ya China, ByteDance, kuuza shughuli mtandao wa TikTok kwa Marekani kwa madai ya usalama wa kitaifa.


Hatua hii inawadia wakati Trump alitia saini agizo kuu wiki iliyopita kutengua marufuku ya Utawala wa Biden kwa TikTok ambayo iliondoa programu hiyo kwa muda mfupi kwa watumiaji wake wa milioni 170 nchini Marekani.

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page