top of page

TOYOTA YAONGOZA KWA KUWA KAMPUNI ILIYOUZA MAGARI MENGI ZAIDI KWA MWAKA 2024

Na VENANCE JOHN


Kampuni ya Toyota Motor leo imesema mwaka jana wa 2024 iliuza magari milioni 10.8, na kubaki kuwa kampuni inayouza zaidi ulimwenguni kwa mwaka wa tano mfululizo. Kampuni hiyo ya kutengeneza magari ya Kijapani imechapisha kushuka kwa asilimia 3.7 katika mauzo.


Licha ya kushuka kwa mauzo, bado imebaki kuwa kampuni iliyouza magari mengi zaidi. Kupungua huko kulichangiwa zaidi na mdororo mkubwa wa mauzo nchini Japani ambapo kampuni hiyo ilikabiliwa na matatizo kutokana na masuala ya utawala kuhusu taratibu za majaribio ya uidhinishaji, hasa katika magari ya matoleo ya Daihatsu.


Kampuni mpinzani wa pili wa Kijerumani Volkswagen Group mapema mwezi huu iliripoti kupungua kwa mauzo kwa 2.3%, katika mauzo mwaka jana hadi zaidi ya magari milioni 9. Mauzo ya magari ya Toyota hasa yale ya majina na chapa ya Lexus, yalishuka kwa 1.4% kutoka mwaka uliotangulia wa 2024 hadi magari milioni 10.2.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page