top of page

TP MAZEMBE WAMEKUJA KUJIFUNZA ILA KUNA WATU JIRANI TU WANAPIGA KELELE HAWANA CHA KUJIFUNZA - ALL KAMWE

Msafara wa Viongozi wa TP Mazembe ukiongozwa na CEO wao, Frederic Kitengie, wamefika Makao Makuu ya Klabu ya @yangasc na kupokelewa na Mtendaji Mkuu wetu, Andre Mtine ambapo wamefika kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali, Afisa Habari wa klabu hiyo Ally Kamwe amesema

"Klabu kubwa kama TP Mazembe imesafiri kutoka DR Congo kuja hapa Jangwani kujifunza



kwa kichwa chetu, Rais wetu Eng. Hersi Said halafu kuna watu wako nyumba ya 16 tu jirani hapo, wanapiga kelele kuwa hawana cha kujifunza kwa Yanga. Niwaambie tu, tutabeba Makombe hadi kila Mwanachama atakuwa anabeba la kuweka nyumbani kwake" @alikamwe

Nae Mkurugenzi wa sheria wa Yanga SC Simon Patrick amefunguka haya

"Tumepokea ugeni mzito kutoka moja ya Klabu kubwa Barani Afrika, TP Mazembe ya DR Congo ambao wamevutiwa na namna Klabu yetu ya Yanga inavyoendeshwa hivyo wamekuja hapa Tanzania kujifunza mambo mbalimbali kwenye Mfumo wetu wa Mabadiliko ya Uendeshaji" Simon Patrick, Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga SC.

"Pia tutakuwa na makubaliano rasmi ya urafiki wa kushirikiana kati ya Klabu yetu ya Yanga na TP Mazembe ili kuweza kubadilisha ujuzi wa mambo mbalimbali ya kimpira yatakayoweza kuisaidia Klabu yetu" Simon Partick, Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga SC.

Kwa upande wake Frederic Kitengie, CEO wa TP Mazembe amesema

Tunafuraha kubwa kufika hapa, ni heshima kubwa kwetu na tumefurahi kwa mapokezi mazuri mliyotupatia, tumekuja hapa kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Yanga na kutengeneza urafiki mzuri utakaoweza kuvisaidia vilabu vyetu hivi viwili bora Afrika Mashariki na kati hivi sasa" Frederic Kitengie, CEO TP Mazembe.

Komentarze


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page