Na VENANCE JOHN
Tovuti ya vituo kadhaa vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Marekani imeondoa seti za data (dataset) zinazohusiana na VVU, watu wa waliobadili jinsi, na tabia za afya ya vijana. Data hizo zimeondolewa baada ya shirika hilo kuagizwa kutii amri ya utendaji kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Donald Trump.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_84eba890690a4745a7631dff8dfa3d89~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_84eba890690a4745a7631dff8dfa3d89~mv2.jpeg)
Mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza na magonjwa ya mlipuko Dk. Jennifer Nuzzo anaeleza kuwa amri hiyo ina athari kubwa akisema kuwa hayo ni maamuzi ya kisiasa na siyo maamuzi ya kisayansi.
Dr. Nuzzo amesema takwimu hizo ni mhimu kupatikana kwa umma kwani zinasaidia mashirika na taasisi za umma kujua ukubwa wa tatizo na hata umma wenyenwe kujua ukubwa wa tatizo na kuchukua hatua za kujilinda.
Amesema kuwa taasisi nyingi zinazojihusisha na afya zinahitaji data kutoka kutuo cha CDC kwa ajili ya kupanga na kuweka bajeti zao ili kutoa huduma kwa jamii, hivyo kuzuia data zisichapishwe kwenye tovuti ni kuziweka taasisi hizo gizani.
Comments