Na VENANCE JOHN
Rais wa Marekani, Donald Trump ametia saini amri ya utendaji ya kuiwekea vikwazo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa kile alichokiita uchunguzi usio na msingi dhidi ya Marekani na mshirika wake wa karibu, Israel.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_6d4f9f641a9d4280be4763b7a9c91f30~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_6d4f9f641a9d4280be4763b7a9c91f30~mv2.jpeg)
Itakumbukwa kuwa mahakama yakimataifa ya uhalifu wa kibinadamu (ICC), ilitoa waranti wa kukamatwa waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wake wa ulinzi Yoav Gallants kuhusiana na vita vya Gaza.
Agizo hilo la Trump la jana Alhamisi limedai kuwa, mahakama ya The Hague ilitumia vibaya mamlaka yake kwa kutoa hati ya kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Amri hiyo pia imedai kuwa, ICC ilijihusisha na vitendo visivyo halali na visivyo na msingi vinavyolenga Marekani na Israel, ikimaanisha uchunguzi wa ICC juu ya uhalifu wa kivita wa Marekani nchini Afghanistan na mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza.
Agizo hilo linajumuisha kuzuiliwa kwa fedha na marufuku ya kusafiri dhidi ya maafisa wa ICC, wafanyakazi, na jama zao, pamoja na yeyote anayekisiwa kwamba alisaidia uchunguzi wa mahakama hiyo.
Comentários