Na VENANCE JOHN
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anatarajia mshirika wake Elon Musk kupata mabilioni ya dola za udanganyifu na utumiaji mbaya katika katika wizara ya ulinzi Pentagon, baada ya kupewa jukumu la kuongoza ukaguzi wa kupunguza ukubwa wa wafanyakazi wa serikali ya Marekani.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_f594bca5d0334d3585eee9174ffc6df8~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_f594bca5d0334d3585eee9174ffc6df8~mv2.jpeg)
"Tutapata mabilioni, mamia ya mamilioni ya dola za ulaghai na matumizi mabaya," Trump alisema katika mahojiano na Fox News. Bajeti ya Pentagon inakaribia dola trilioni 1 kwa mwaka. Bilionea wa mrengo wa kulia na bosi wa SpaceX na Tesla, Elon Musk, ambaye Ikulu ya Marekani ilimteua kuongoza Idara mpya ya Ufanisi wa Serikali (DOGE), atapata taarifa za siri katika mifumo ya kompyuta katika mashirika mbalimbali ya serikali ili kutimiza kazi aliyoteuliwa kufanya.
Viongozi kutoka katika wigo wa kisiasa kwa muda mrefu wamekosoa ubadhirifu na uzembe katika Pentagon, lakini wakosoaji wanasema juhudi hizi zinahatarisha kufichua habari za siri na kuharibu mashirika yote bila idhini ya bunge.
Makampuni ya Musk pia yana kandarasi kuu na Pentagon, ambayo imeibua wasiwasi mkubwa wa mgongano wa maslahi. Jaji wa Marekani Jumamosi alitoa amri ya dharura ya kuzuia DOGE kufikia mifumo ya malipo ya Idara ya Hazina ambayo ina data nyeti za Wamarekani.
Comments