top of page

TRUMP AMWAMBIA MFALME WA JORDAN KUWA GAZA ITAKUWA MALI YA MAREKANI, HII NI MARA YA TATU KUSISITIZA

Na VENANCE JOHN


Rais wa Marekani, Donald Trump kwa mara nyingine amesisitiza kuwa Marekani itachukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza. Trump amesema hayo jana alipokutana na Mfalme Abdullah wa Jordan katika Ikulu ya White House.


Ulikuwa ni mkutano wao wa kwanza tangu Trump atangaze pendekezo lake la kuchukua eneo hilo na kuwahamisha Wapalestina milioni mbili na kuwapeleka nchi nyingine za kiarabu, ikiwemo Jordan.


Mapema wiki hii, Trump alipendekeza kuwa anaweza kuzuia msaada kwa Jordan na Misri isipokuwa wakubali kuwachukua Wapalestina hao kutoka Gaza. Jordan, mshirika mkuu wa Marekani katika Mashariki ya Kati, tayari ni nyumbani kwa mamilioni ya Wapalestina na imekataa pendekezo la Trump la kuichukua Gaza.


Mfalme Abdullah alisema baada ya mkutano wao kwamba msimamo thabiti wa Jordan ni kupinga kuhama kwa Wapalestina kutoka katika Ukanda wa Gaza. Lakini Trump akizungumza na waandishi habari, huku Mfalme Abdullah akiwa ameketi upade wake wa kulia, Trump aliashiria hatabadili wazo lake ambalo limezua shutuma za kimataifa.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page