Na VENANCE JOHN
Rais wa Marekani Donald Trump amekubali kusitisha kutoza ushuru wa 25% kwa Canada na Mexico kwa siku 30, na kuondoa kwa muda vita vya kibiashara vinavyoweza kuongezeka. Baada ya simu za dakika za mwisho kati ya Trump na Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau alikubali kuimarisha mpaka wa nchi yake na Marekani ili kudhibiti uhamiaji na mtiririko wa dawa hatari ya fentanyl.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_456a25e4462440a691802401f9c84cfd~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_456a25e4462440a691802401f9c84cfd~mv2.jpeg)
Hapo awali, Trump alifanya makubaliano na Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum. Alikubali kuimarisha mpaka wa kaskazini na askari. Kwa upande wake Marekani ingepunguza uingiaji wa bunduki kutoka nchini Mexico. Lakini ushuru wa 10% wa Marekani kwa bidhaa kutoka China umeanza kutumika, baada ya tarehe ya mwisho ya leo Jumanne usiku kupita.
Muda mfupi baadaye, China nayo imetangaza kuwa inatoza ushuru wa kulipiza kisasi kwa bidhaa nyingi za Marekani, ikiwa ni pamoja na 15% kwa makaa ya mawe na gesi asilia iliyoyeyuka na 10% kwa mafuta yasiyosafishwa na mashine za kilimo. Hapo awali Trump alisema kuwa anapanga kuzungumza kwa simu na rais wa China hivi karibuni.
Comments