Na VENANCE JOHN
Rais wa Marekani, Donald Trump, amependekeza kuwa ukanda wa Gaza uwe chini ya udhibiti wa Mareakani na kwamba watu milioni 1.8 wa Gaza wahamishwe kwenda nchi nyingine za Kiarabu. Trump alitoa pendekezo hilo akiwa na waziri mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu, katika mkutano na waandishi habari ambapo Netanyahu yuko ziarani jijini Washington, Marekani.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_c8707f0e885645edb63486e6cd0d8420~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_c8707f0e885645edb63486e6cd0d8420~mv2.jpeg)
Trump amesema baada ya Marekani kuijenga upya Gaza, inaweza kuwa makazi ya watu wa dunia nzima. Alipoulizwa na wanahabari ni kwa mamlaka gani Marekani inaweza kuchukua udhibiti wa Gaza, Trump hakujibu moja kwa moja, lakini amesema anaona kuwa kuna hati miliki ya muda mrefu.
Netanyahu alikubaliana na wazo la Trump na kumuita rais huyo rafiki mkubwa wa Israel. Vile vile Trump alimkosoa mtangulizi wake Joe Biden akidai aliruhusu maadui wa Israel kuwa na nguvu zaidi katika kipindi chake cha miaka minne madarakani.
Mapema, hata kabla ya pendekezo hilo, msemaji wa kundi la Hamas ambalo ndilo lenye utawala ukanda wa Gaza alikosoa pendekezo hilo, akisema ni mpango wa kuleta machafuko na kusisitiza kwamba watu wa Gaza hawataruhusu mipango hiyo.
Commentaires