top of page

TRUMP ASAINI SHERIA YA KUIPIGA MARUFUKU WHO NHINI MAREKANI

Na VENANCE JOHN


Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini, amri ya kuanza mchakato wa kuiondoa Marekani kuwa mwanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Trump amesema kuwa hilo ni jambo kubwa na alitoa kauli hiyo alipokuwa akiidhinisha hati hiyo baada ya kurejea tena katika Ikulu ya Marekani.


Ilikuwa ni moja ya amri kadhaa za utendaji alizotia saini siku ya kwanza madarakani. Hii ni mara ya pili kwa Trump kuamuru Marekani kujiondoa kuwa mwanachama wa WHO. Trump alikosoa jinsi WHO lilivyoshughulikia janga la Covid-19 na kuanza mchakato wa kujiondoa kutoka kwa taasisi hiyo ya Geneva wakati wa janga hilo. Baada ya Trump kushindwa katika uchaguzi na Joe Biden, Rais Joe Biden baadaye alibatilisha uamuzi huo.


Agizo hilo linasema Merekani inajiondoa kwa sababu ya WHO kutoshughulikia janga la Covid-19 ambalo liliibuka Wuhan, China, na majanga mengine ya afya ya ulimwengu, kushindwa kwake kupitisha mageuzi yanayohitajika haraka, na kutokuwa na uwezo wa kuonyesha uhuru kutoka kwa mambo yanayohitaji uhuru kutoka kwa ushawishi wa kisiasa wa nchi wanachama wa WHO. Trump alipokuwa bado ofisini kwa mara ya kwanza alikosoa shirika hilo kwa kuwa kuipendelea China katika kukabiliana na janga la Covid-19.

Commenti


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page