top of page

TRUMP ASEMA HAMAS INAPASWA KUWAACHILIA MATEKA WOTE IFIKAPO JUMAMOSI MCHANA AU KIAMA KIZUKE

Na VENANCE JOHN


Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Hamas inapaswa kuwaachilia mateka wote wanaoshikiliwa na kundi hilo ifikapo Jumamosi adhuhuri (mchana) la sivyo atapendekeza kufutwa kwa usitishaji vita kati ya Israel na Hamas na kuacha kuzimu izuke.


Trump ametahadharisha kuwa huenda Israel ikataka kupuuza suala hilo na akasema huenda akazungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Lakini katika kikao kikubwa na waandishi wa habari katika, Trump hapo jana alionyesha kuchoshwa na hali ya kundi la mwisho la mateka walioachiliwa huru na Hamas na kwa tangazo la kundi hilo la wanamgambo kwamba litasitisha kuwaachilia mateka zaidi.


"Ninachofahamu, kama mateka wote hawatarejeshwa kufikia Jumamosi saa 6 kamili mchana, nadhani ni wakati mwafaka. Ningesema, ghairi na dau zote zimezimwa na kuzimu na kiama kizuke. Ningesema wanapaswa kurejeshwa ifikapo saa sita Jumamosi," Trump alisema.


Alisema alitaka mateka waachiliwe kwa wingi, badala ya wachache kwa wakati mmoja. "Tunataka wote warudi." Alisema Trump. Trump pia amesema huenda akazuia msaada kwa Jordan na Misri ikiwa hawatachukua wakimbizi wa Kipalestina wanaohamishwa kutoka Gaza. Trump atakutana na Mfalme Abdullah wa Jordan siku ya Jumanne.


Maoni hayo yalikuja siku ya mkanganyiko juu ya pendekezo la Trump kurudia tena nia yake ya kutaka kuimili Gaza mara tu mapigano yatakapokoma. Trump amesema Wapalestina hawatakuwa na haki ya kurejea Ukanda wa Gaza chini ya pendekezo lake la kulijenga upya eneo hilo, akipingana na maafisa wake ambao walipendekeza Wagaza watahamishwa kwa muda tu.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page