top of page

TRUMP ASEMA KUANZIA KESHO CANADA NA MEXICO ZITAANZA KUTOZWA USHURU WA 25%

Na VENANCE JOHN


Rais wa Marekani Donald Trump amerudia ahadi yake ya kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za Canada na Mexico kuanzia kesho Jumamosi. Hata hivyo Trump amesema kwamba uagizaji wa mafuta unaweza kusamehewa ushuru huo.


Akizungumza na waandishi habari katika Ikulu ya White House hapo jana, Trump amesema kwa sasa anaweza au asiweze kuyatenga mafuta kutoka kwenye ushuru na kwamba angeamua pengine usiku wa leo.


"Tutafanya uamuzi huo labda usiku wa leo kwa mafuta," Trump alisema. Canada na Mexico zote zimeahidi kujibu ushuru wa Marekani kwa namna Fulani. Trump pia amesema kwamba anazingatia ushuru wa asilimia 10 kwa China ili kuishinikiza Beijing kusitisha usambazaji wa kemikali ya fentanyl. "Kwa hivyo China itaishia kulipa ushuru pia kwa hilo, na tuko katika mchakato wa kufanya hivyo," Trump amesema.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page