Na VENANCE JOHN
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini kwamba Marekani, inapiga hatua katika mazungumzo yake ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine. Hata hivyo Rais Trump amekataa kutoa maelezo kuhusu mawasiliano yoyote aliyoyafanya na Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu suala hilo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_a771b6dc361546b7857f1a43772b5c6b~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_a771b6dc361546b7857f1a43772b5c6b~mv2.jpeg)
Akizungumza na waandishi habari ndani ya ndege ya Air Force One wakati akielekea katika mchezo wa Super Bowl, Trump alidokeza kuwa yeye na Putin walikuwa wakiwasiliana na kwamba anatarajia kufanya mazungumzo zaidi. Trump ameongeza kuwa Marekani inawasiliana na pande zote mbili za Urusi na Ukraine na kuahidi kumaliza vita ingawa lakini bado haijawekwa wazi jinsi atakavyofanikisha suala hilo.
Comments