Na VENANCE JOHN
Rais wa Marekani, Donald Trump ametumia karibu siku nzima kumshambulia Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na kumwita dikteta. Mnyukano huo unazidi kuongeza mvutano kati ya viongozi hao wawili.

Kauli ya Trump inakuja baada ya kauli ya Zelensky, alivyojibu mazungumzo kati ya Marekani na Urusi huko Saudi Arabia ambapo Ukraine haikushirikishwa, akisema kuwa rais wa Marekani alikuwa anadanganywa na Urusi.
Akizungumza katika mkutano wa uwekezaji unaoungwa mkono na Saudi Arabia huko Florida, Trump amesema jambo moja tu ambalo Zelensky alikuwa mzuri ni kumchezea mtangulizi wake Joe Biden.
Hata hivyo viongozi wa Ulaya kwa haraka walikosoa matamshi kwa Trump, akiwemo Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, ambaye amesema, ni jambo lisilo sahihi na hatari kukanusha uhalali wa kidemokrasia wa Rais Zelensky.
Naye waziri mkuu wa Uingereza, Sir Keir Starmer, ameweka wazi kuwa anamuunga mkono Zelensky huku waziri mkuu wa Sweden, Ulf Kristersson, akikosoa matumizi ya neno dikteta kulikofanywa na Trump na waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, akisema kauli hizo hazina maana.
Comments