top of page

TRUMP ATIA SAINI AGIZO LA UTENDAJI KURUHUSU MIRIJA YA PLASTIKI KUANZA KUTUMIKA TENA

Na VENANCE JOHN


Rais Donald Trump ametia saini agizo kuu linalolenga kuhimiza serikali ya Marekani na watumiaji mirija ya plastiki, kitendo ambacho ni kurudisha nyuma juhudi za mtangulizi wake za kuondoa matumizi ya plastiki. "Tunarejea kwenye mirija ya plastiki," Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House alipokuwa akitia saini agizo hilo, akisema kwamba mirija ya karatasi haifanyi kazi.


"Sidhani kama plastiki itaathiri papa sana, kwani wanapitia baharini," Trump alisema. Mtangulizi wa Trump, Rais Joe Biden, alikuwa amependekeza hatua za kimazingira kupunguza matumizi ya plastiki isiyoweza kuharibika kwa matumizi yamara moja tu, ambayo huharibu mifumo ya ikolojia na kuchafua usambazaji wa chakula.


Amri ya utendaji ya jana Jumatatu ilikuwa sehemu ya kudhoofisha kwa mapana zaidi ahadi za mazingira na Trump, ambaye katika moja ya vitendo vya kwanza vya muhula wake wa pili, aliondoa Marekani kutoka kwa makubaliano ya hali ya hewa ya Paris kwa mara ya pili.


Trump pia alibatilisha sera ya utawala ya Biden ya kukomesha matumizi ya bidhaa zote za plastiki zinazotumiwa mara moja kwenye ardhi ya Marekani ifikapo 2032. Nchi nyingi zimepiga marufuku aina mbalimbali za plastiki zinazotumika mara moja, zinazozalishwa hasa kupitia kemikali za petroleum na zinazotumiwa kutengeneza mifuko ya ununuzi, chupa na vitu vingine vinavyoweza kutumika.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page