Na VENANCE JOHN
Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri ya utendaji hapo jana ya kukabiliana na chuki dhidi ya Wayahudi na kuahidi kuwafukuza wanafunzi wa vyuo vikuu wasio raia na wengine walioshiriki katika maandamano ya kuunga mkono Palestina.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_97fe2b4698f94774acf393d8fc55b4bb~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_97fe2b4698f94774acf393d8fc55b4bb~mv2.jpeg)
Amri hiyo ni kupambana na kile ilichokiita mlipuko wa chuki dhidi ya Wayahudi kwenye vyuo vikuu na mitaanui. "Kwa wakazi wote wa kigeni waliojiunga na maandamano ya wafuasi wa jihadi, tunawataarifu: njooni 2025, tutawapata, na tutawafukuza," Trump alisema kwenye nyaraka hiyo aliyotia saini.
Nyaraka hiyi, inaeleza kuwa ataghairi haraka visa za wanafunzi wa wafuasi wote wa Hamas kwenye vyuo vikuu, ambavyo vimeshambuliwa na itikadi kali kuliko hapo awali tamko hilo likiwa ni ahadi ya kampeni yake ya urais 2024. Mashirika ya haki za binadamu na wasomi wa sheria walisema hatua hiyo mpya itakiuka haki za uhuru wa kujieleza za kikatiba na huenda ikaleta changamoto za kisheria.
Comments