top of page

TRUMP ATISHIA KUJIONDOA KWENYE MDAHALO NA KAMALA HARRIS, ATOA MASHARTI

Na VENANCE JOHN


Timu ya kampeni ya Donald Trump na Kamala Harris zimepambana leo Jumatatu kuhusu namna ambavyo mdahalo wa wagombea urais nchini Marekani unavyotakiwa kufanyika.


Timu ya makamu wa rais Kamala Harris inataka kuzimwa vinasa sauti (microphone/maiki) huku mpinzani wake wa chama cha Republican Bw. Donald Trump akitishia kujiondoa kabisa, na kutopendekeza runinga ya ABC iliyokubaliwa hapo awali kuendesha mdahalo huo kwani runinga hiyo awali ililaumiwa kwa upendeleo.


"Kwa nini nifanye mdahalo dhidi ya Kamala Harris kwenye runinga hiyo?" Trump, ambaye anasaka nafasi ikulu ya White House, aliandika katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii huku akiishutumu runinga ya ABC kwa upendeleo. Mshauri mkuu wa kampeni ya Trump, Bw. Jason Miller amesema kuwa tayari wamekubaliana na masharti yaliyo sawa na mdahalo wa Juni ulioendeshwa na runinga ya CNN.


Katika mdahalo wa mwezi Juni ambao uliwakutanisha Trump na Joe Biden, ulikuwa una masharti ya kuzima vinasa sauti (microphone) kwa kuwa Trump alihofiwa kuwa angeongea hata wakati ambao mwenzake Joe Biden alikuwa anaongea.


Lakini Trump baadaye aliwaambia waandishi wa habari kwamba angependelea kuwa na kinasa sauti chake, akiongeza kwamba hakupenda mdahalo kati yake na Joe Biden kwani vinasa sauti vilikuwa vimezimwa.


Huku fukuto hilo likiendelea wagombea wa umakamu wa rais, Seneta wa chama cha Republican JD Vance na Gavana wa Minnesota, Tim Walz, wameratibiwa kufanya mdahalo Oktoba 1 kupitia runinga ya CBS.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page