top of page

TRUMP ATISHIA KUTWAA TENA UDHIBITI WA MFEREJI WA PANAMA (PANAMA CANAL)

Na VENANCE JOHN


Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametishia kuweka tena udhibiti wa Marekani juu ya Mfereji wa Panama, akiishutumu nchi ya Panama kwa kutoza viwango vya kupita kiasi kikubwa pesa cha kutumia njia ya Amerika ya Kati.


Akizungumza na umati wa wafuasi huko Arizona, Trump pia amesema hataruhusu mfereji huo uanguke kwenye mikono mibaya, akionya juu ya uwezekano wa ushawishi wa China kwenye njia hiyo.


Kauli hiyo ya Trump imekemewa vikali kutoka kwa Rais wa Panama Jose Raul Mulino. "Ikiwa kanuni, za kimaadili na za kisheria, hazitafuatwa, basi tutadai kwamba Mfereji wa Panama urudishwe kwetu, kwa ukamilifu, haraka na bila swali." Trump alisema


Katika ujumbe uliorekodiwa uliotolewa na Rais wa Panama Mulino siku ya naja Jumapili alasiri, kiongozi wa taifa hilo alisema kuwa uhuru wa Panama haujadiliwi na kwamba China haina ushawishi kwa usimamizi wa mfereji huo. Rais Mulino pia alitetea viwango vya pesa vya kupitia njia hiyo ilivyotozwa na Panama, akisema havikuwekwa kwa matakwa au shinikozo kutoa kwa nchi nyingine.


China haidhibiti wala kusimamia mfereji huo, lakini kampuni tanzu ya CK Hutchison Holdings yenye makao yake Hong Kong kwa muda mrefu imesimamia bandari mbili zilizo kwenye lango la viingilio vya mfereji wa Karibea na Pasifiki.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page