top of page

TRUMP ATOA MSAMAHA KWA WANAHARAKATI WANAOPINGA UTOAJI MIMBA, LEO KUWAHUTUBIA

Na VENANCE JOHN


Rais wa Marekani Donald Trump ametoa msamaha kwa wanaharakati wanaopinga uavyaji mimba (utoaji mimba) 23 waliokuwa wanasota jela. Mmoja wa walioripotiwa kusamehewa ni Lauren Handy ambaye mwaka 2020 alikuwa kiongozi wa kikundi cha Progressive Anti-Abortion Uprising (PAAU) ambaye anajielezea kama mkatoliki mhafidhina.


Tarehe 22 Oktoba mwaka huo, Handy alipanga miadi kwa kujifanya kama anataka kuavya mimba katika kliniki ya Upasuaji ya Hazel Jenkins huko Washington DC. Alipofika, yeye na wengine walilazimisha kuingia ndani ya kliniki hiyo na katika purukushani hizo muuguzi (nurse) mmoja aliteguka kifundo cha mguu.


Handy alikamatwa na kushtakiwa kwa kula njama ya kujeruhi, kukandamiza, kutishia na kutisha wagonjwa na wafanyakazi na alipatikana na hatia mwezi Agosti 2023 na kuhukumiwa miaka mitatu ya kifungo cha nje lakini chini ya usimamizi.


Leo hapo baadaye Rais Donald Trump anatarajiwa kuhutubia kupitia video mkutano mkubwa wa kila mwaka wa kupinga uavyaji mimba nchini Marekani. Mwaka 2020, Trump alikua rais wa kwanza wa Marekani kuhudhuria mkutano huo ana kwa ana.


Marais wa awali kupitia chama cha Republican, akiwemo George W Bush na Ronald Reagan, wamehutubia kundi hilo kwa mbali. Maandamano ya kila mwaka yalianza kwa mara ya kwanza mwaka 1974 mwaka mmoja baada ya Mahakama ya Juu ya Marekani kuhalalisha utoaji mimba sheria iliyopewa jina la Roe v Wade.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page