Na VENANCE JOHN
Rais Donald Trump leo amesema kwamba ana mpango wa kuwaondoa zaidi ya watu 1,000 walioteuliwa kutoka kwa utawala wa Rais wa zamani Joe Biden. Trump ametangaza kuwafuta kazi wanne wa kwanza kwenye mitandao ya kijamii, akiwemo mpishi mashuhuri Jose Andres na jenerali mkuu wa zamani Mark Milley.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_28b9cc8a13bf422c8cc602f62c49fd16~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_28b9cc8a13bf422c8cc602f62c49fd16~mv2.jpeg)
"Ofisi yangu ya Utumishi wa Rais iko katika mchakato wa kuwatambua na kuwaondoa zaidi ya Wateule elfu moja wa Rais kutoka kwa Utawala uliopita, ambao hawaambatani na maono yetu ya Kufanya Marekani kuwa Kubwa Tena," Trump alisema katika chapisho kwenye mtandao wa Truth Social baada ya saa sita usiku.
Hatua hiyo huenda ikazua wasiwasi kwamba rais analenga kuchukua nafasi ya walioteuliwa na Biden na watu binafsi wanaoamini ajenda yake. Andres, ambaye alitunukiwa Nishani ya Urais ya Uhuru na Biden, ameondolewa kwenye Baraza la Rais la Michezo, Usawa na Lishe, Trump amesema.
Picha ya Milley, ambaye Trump amependekeza anyongwe kwa sababu alifanya mazungumzo na China, picha yake iliondolewa kutoka Pentagon muda mfupi baada ya kuapishwa kwa Trump. "Hebu hii iwe kama Notisi Rasmi ya Kufukuzwa kazi kwa watu hawa 4, na wengi zaidi, wanakuja hivi karibuni," Trump aliandika, na kuongeza: "UMEFUKUZWA KAZI!"
Trump pia aliamuru wafanyikazi wa shirikisho kurejea ofisini siku tano kwa wiki. Washirika wa Trump wamesema mamlaka ya kurejea kazini na kuondolewa kwa ulinzi wa utumishi wa umma unaojulikana sana kama "Ratiba F", inakusudiwa kumsaidia rais kuchukua nafasi ya wafanyakazi wa serikali waliokaa kwa muda mrefu na wafuasi.
Comments