top of page

TRUMP AZUNGUMZA NA PUTIN KUMALIZA VITA VYA UKRAINE, ASEMA UKRAINE INAWEZA ISIPATE ARDHI YAKE YOTE ILIYO CHINI YA URUSI

Na VENANCE JOHN


Rais wa Marekani Donald Trump amesema alikuwa na mazungumzo ya simu ya muda mrefu na yenye tija kubwa na rais wa Urus Vladimir Putin hapo jana ambapo viongozi hao walikubali kuanza mazungumzo ya kumaliza vita nchini Ukraine.


Katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump amesema yeye na rais wa Urusi wamekubali timu zao zianze mazungumzo mara moja na kualikana kila mmoja kutembelea mji mikuu wa mwenzake. Baadaye, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema alikuwa amezungumza na Trump kuhusu amani ya kudumu na ya kutegemewa.


Wakati wa maelezo mafupi ya Rais wa Marekani Donald Trump kwa waandishi wa habari katika Ikulu ya White House hapo awali, alipoulizwa namna mipaka ya Ukraine inavyoweza kuonekana ikiwa vita vitaisha


Aliulizwa, Je ramani zingeonekana kama zilivyokuwa kabla ya 2014? Trump Naye akajibu; "hakika inaweza kuonekana kuwa haiwezekani". Na kuongeza; "Walichukua ardhi nyingi na walipigania ardhi hiyo, na walipoteza askari wengi." Trump ameongeza kuwa baadhi ya ardhi hiyo ingerudi kwa Ukraine.

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page